Alizaliwa kama Dwayne Michael Carter, Jr. na kukulia mjini Hollygrove karibu kidogo na mji wa New Orleans, Louisiana. Akiwa na umri wa miaka kumi na moja, akakutana na Bryan Williams, rapa na ndiyo mmiliki wa studio ya Cash Money Records. Baada ya makutano hayo, Wayne akarekodi rap flani ya michano katika studio hiyo ya Williams kwa kutumia chombo maalum cha kuweza kukujibu wakati unachana. Na kwa bahati nzuri michano hiyo ilimwacha hoi mmiliki huyo wa studio na kuthubutu hata kumwingiza Wayne katika studio yake. Wayne pia ana mtoto wa kike mmoja aitwaye Reginae Carter, aliyezaa na Bi. Antonia "Toya" Johnson, demu wake wa kitambo toka shule. Wawili hao walikuja kuoana wakati ule wa Siku Kuu ya Wapendanao ya mwaka wa 2004, lakini wawili hao walikuja kutarikiana mnamo mwaka wa 2006.